Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya
dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo
katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminal One) Dar es salaam.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya
kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za
sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.
Maafisa
wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa
wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria
katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu
utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli
aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola
kuchukua hatua mara moja.
“Unajua
mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini
nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sasa sipendi kudanganywa,
ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio
mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu
mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi
miwili." Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege
“Kwa
hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa
hiyo mtu nikiamua kuja na madawa yangu ya kulevya, nikaja na dhahabu
zangu, na almasi zangu na meno ya tembo kwa kutumia hizi ndege
ndogondogo napita tu” Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara hii ya kushtukiza mara baada ya
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea
Jijini Kampala nchini Uganda ambako jana alihudhuria sherehe ya
kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.
0 comments:
Post a Comment