Zari akiwa na marafiki zake, Dj Zihle na Nohle
Unakumbuka kipindi kile Diamond na Zari wameenda Ulaya kwenye ziara ya
‘From Tandale to the World’ na ex wa Zari, Ivan kudai naye anaipeleka
familia yake kula bata Ibiza ambako hakwenda hata hivyo?
Mganda huyo tajiri anayeishi Afrika Kusini na aliyezaa watoto watatu
na Zari haishiwi vibweka na vimbwanga! Ni kwasababu sasa amekuja na
kingine kilichochoea mjadala mpya kwenye mitandao ya kijamii wa kama
bado wawili hao wanaonana zaidi ya inavyotakiwa.
Siku kadhaa zilizopita, Zari alipost picha akiwa kwenye swimming pool
akifurahia maji vugu vugu na marafiki zake wa South ambao nao ni
mastaa, Dj Zinhle ambaye ni ex wa rapper AKA na mama wa mtoto wake
pamoja na Nohle Ndala.
“This is the life, what you living i don’t know what it is….,” ameandika katika post moja wapo.
Watatu hao walikuwa kwenye sehemu inaitwa Soulstice Day Spa ya
Capetown, Afrika Kusini. Ni sehemu ya kifahari ambapo watu huenda kupata
huduma mbalimbali zikiwemo massage.
Wiki hii Ivan kawachakua pia washkaji zake na kwenda kubarizi hapo na
hivyo picha zake kuleta utata kwa watu ambao hawafahamu kuwa hiyo ni
sehemu public ambayo mtu yeyote anaweza kwenda.
0 comments:
Post a Comment