Hatimaye mjane aliyemwaga machozi mbele ya Rais John Magufuli akidai
kudhulumiwa mali ya urithi, amepewa nyumba na shamba baada ya Mkuu wa
Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Crispin Meela kusuluhisha mgogoro wa
umiliki wa mali hizo.
Hivi karibuni akiwa mjini Babati, Rais
Magufuli alimuagiza Meela ahakikishe mjane huyo, Mwanaidi Mussa anapewa
mali zake ikiwamo nyumba na shamba zilizokuwa zinadaiwa kuchukuliwa na
mke mdogo kinyume cha sheria.
Meela alimkabidhi nyumba na shamba
la ekari 2.5 mjane huyo juzi na kuagiza mke mdogo kama hakuridhika na
uamuzi, akakate rufaa mahakamani.
Meela pia aliwataka wananchi
kuacha kurubuniwa na watu wachache wenye maslahi binafsi na badala yake
wafuate maelekezo yanayotolewa na vyombo vya sheria.
“Migogoro
ya mirathi imeendelea kukithiri katika maeneo mengi nchini kutokana na
watu kutofuata sheria za mirathi na wengine wakitaka kunufaika na mali
zinazoachwa na marehemu,” alisema Meela.
Mwanaidi ambaye
amezeeka, alidai kwa muda mrefu amewaomba viongozi wa Serikali ya mtaa
anaoishi wamsaidie, kutatua tatizo lake lakini walimpuuza.
Mke
mdogo, Asia Musa alidai kuwa nyumba hiyo aliyokabidhiwa Mwanaidi,
aliijenga na mumewe kauli ambayo ilikinzana na ya mke mkubwa aliyedai
kuwa wakati Asia anaoelewa alikuta nyumba ameshaijenga na mumewe.
0 comments:
Post a Comment