Jeshi
la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za
kukamatwa wakiwa wanatoa fedha benki ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha
shilingi 3,680,000 wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja
na namba za siri za kadi hizo. .
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amesema watuhumiwa
hao watatu walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku katika Tawi la NMB
Mpanda .
Watuhumiwa
hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea,
wamekamatwa na askari wa jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo.
Nyanda
ameeleza kuwa watumiwa walikamatwa baada ya askari polisi kuwatilia
mashaka kutokana na kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha
mashine ya kutolea fedha .
Amesema
baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho na
kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kutoa fedha katika mashine
tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea fedha.
Kaimu
Kamanda alieleza ndipo askari polisi walipoamua kuwapekua watuhumiwa na
waliwakuta wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na
namba za siri za kadi h izo na walikuwa tayari wameishatoa kiasi cha
fedha taslimu shilingi 3,680,000.
Amezitaja
Namba za Kadi za ATM walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni AC
61908000058,AC 61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC 61902240100,AC
61908000237, AC 61902400518 AC 61910000645, AC 61910004240,AC
61908000609 AC 61902403168.
Kaimu
kamanda Nyanda amezitaja kadi za ATM zingine zilizokamatwa kuwa ni
zenye namba AC 61910000537,AC 61902402653, AC 61910000250, Ac
61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na AC
70408100131.
Amesema
watuhumiwa wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa
tukio hilo kukamilika na bado watuhumiwa wote watatu wanaendelea
kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi .
Kaimu
kamanda ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa siri kwa watu za
namba zao za siri za kadi wanazozitumia kwenye ATM za benki .
0 comments:
Post a Comment