Pichani ni makaburi yakiandaliwa kwaajili ya kuzikwa kwa miili saba ya familia moja mapema leo Wilayani Sengerema.
Mhe. Makamu wa Rais leo ametembelea Wilaya ya Sengerema
kata ya Sima ambapo usiku wa kuamkia jana kulifanyika mauwaji ya
kinyama ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa
kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.
Mhe. Makamu wa Rais Mama Suluhu
Hassan ametoa masaa 24 kwa uongozi wa mkoa wa Mwanza pamoja na jeshi la
polisi na vyombo vingine kuwatia nguvuni wale watu wote waliohusika na
mauaji hayo.
Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu akisalimiana na kuwapa pole ndugu jamaa na
marafiki kufuatia mauaji hayo ya watu wilayani Sengerema
Mkuu
wa Wilaya ya Sengerema Bi Zainab Telack pamoja na Mkuu wa mkoa wa jiji
la Mwanza Mh.John Mongella wakiwa na Mgeni wao Makamu wa Rais Mh.Samia
Suluhu alipokewenda kutoa pole kwenye tukio la mauwaji ya kinyama ya
watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa
mapanga na watu wasiojulikana ndani ya wilaya hiyo katika kijiji cha
Sima mkoani Mwanza.
Makamu
wa Rais Mh Samia Sulluh akizungumza kwenye tukioa la mauwaji ya kinyama
ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa
mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Mh.Samia ametoa sa a 24 kukamatwa
kwa wale wote waliohusika na tukio hilo la Kinyama.
0 comments:
Post a Comment