KAMBI rasmi ya upinzani Bungeni inalaani kitendo cha serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutumia nguvu za kijeshi kutisha
wananchi wa Zanzibar na kutumia mwanya huo kuchakachua mchakato wa
kidemokrasia wa uchanguzi.
Juma Hamad msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wa wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, ameyasema hayo leo Bungeni wakati akiwasilisha maoni ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Amesema serikali itafakari upya matumizi sahihi ya Jeshi
kulishirikisha katika mchakakato wa kutwaa madaraka ya dola kwa njia za
ujanja ujanja ni hatari kubwa.
Hamad amesema kumezuka tabia ya watawala kulitumia Jeshi la Wananchi
katika masuala ya ndani ya kisiasa ili kutimiza matakwa yao ya kisiasa
kitendo ambacho kinadumaza demokrasia katika taifa.
Ametoa mfano kinapofika kipindi cha uchaguzi,
Zanzibar inakuwa kama vile nchi iliyovamiwa kijeshi (invaded country)
vikosi vya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi, na Mgambo kutoka
Tanzania bara vinapelekwa Zanzibar na kupiga makambi kwenye viwanja vya
ndege, bandarini na kwenye vituo vya redio.
Aidha amesema vikosi hiyo vimekuwa vikipita mitaani na wakati
mwingine kufanya mazoezi ya kijeshi katika maeneo ya makazi ya wananchi
jambo ambalo huzua hofu kwa wananchi na kutoa taswira kama vile nchi
inakabiliwa na vita.
Amesema wanatambua kwamba ulinzi wa raia na mali zao unafanywa na
Jeshi la Polisi isipokuwa Jeshi la Ulinzi linaweza kuongeza nguvu ikiwa
tu nchi iko vitani au kama hali ya hatari imetangazwa.
“Ni kwa nini Jeshi la Wananchi wa Tanzania likafanye kazi ya Jeshi la
Polisi huko Zanzibar wakati Jeshi la Polisi lipo, nchi haipo vitani na
pia hakuna hali ya hatari iliyotangazwa”.amesema Hamad.
“Ni vizuri demokrasia iachwe ichukue mkondo wake. Kwa maana hiyo,
Jeshi libakie kulinda mipaka ya nchi yetu na kuilinda Serikali
itakayowekwa madarakani na wananchi wenyewe”.amesema.

0 comments:
Post a Comment