Na Tiganya Vincent, MAELEZO--Dodoma
Wizara
ya Ulinzi na Kujeshi la Kujenga Taifa imepanga kuendelea kuliimarisha
na kuliongezea uwezo Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania kwa
kulipatia vifaa na zana za kisasa pamoja na kutoa mafunzo stahiki ili
kuwa tayari kukabiliana na adui wa ndani na nje.
Mpango
wa Serikali umetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mh.Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akiwasilisha hotuba
kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa
2016/17.
Alisema
kuwa sanajari na hili , Wizara itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa
Wanajeshi nchini ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa huduma na mahitaji ya
msingi kama vile chakula , tiba, sare , usafiri na stahili zao.
Mh.
Dkt. Mwinyi aliongeza kuwa Wizara itaimarisha uwezo wa Jeshi katika
utafiti na kuendeleza teknolojia kwa madhumuni ya kuisaidia uzalishaji
wa bidhaa na huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia hapa nchini na nje
ya nchi.
Aidha
, alisema kuwa Wizara kupitia Jeshi la Kujenga la Taifa itaendelea
kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya uzalendo , umoja wa Kitaifa ,
ukakamavuna kuwapatia stadi za kazi ili kuwaandaa katika uzalishaji
mali.
Dkt.
Mwinyi alisema Wizara kupitia Jeshi litaendelea kuimarisha ushirikiano
wa kijeshi na kiulinzi na nchi nyingine duniani kupitia Jumuiya za
Kimataifa , Kikanda na ushirikiano na nchi moja moja.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Husein
Ali Mwinyi ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuidhinisha jumla shilingi trilioni 1.7 (1,736,530,413,000.00) kwa ajili
ya matumizi ya kawaidia na matumizi ya maendeleo.
Alisema
kati ya fedha hizo shilingi trilioni 1.4 ni kwa ajili ya matumizi ya
kawaida na bilioni 248 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
0 comments:
Post a Comment