Msanii kutoka kiwanda cha Bongo Movie, Diana Nsumba maarufu kama Chodry
amesema kuwa waaigizaji wengi wa kike hapa bongo ni washamba sana.
Diana ambaye anamiliki kampuni ya Twins Film Production
ameshafanikiwa kufanya filamu kadhaa ambazo zimefanya poa kama
‘Julieth’, ‘Only You’ na ‘The Same Script’.
Akizungumza na Bongo5, Chodry amesema, ‘Wasanii wengi wa kike
wakifanya filamu moja wakitokeza kidogo kwenye cover wanaanza matusi
mitandaoni’.
“Mimi huwa nawashangaa sana waigizaji wenzangu, kuna wale ambao
wakiwekwa kwenye cover ya filamu mara moja tu wanaanza kujiona na kuanza
matusi mitandaoni.
Mimi nimeshafanikiwa kufanya kufanya filamu na
wasanii kama JB, Hemedy phd, na wengine wengi lakini hata siku moja
sijaweza kumdharau mtu.
Nawashauri wasanii wenzangu wa kike wenye tabia
hiyo tubadilike ndiyo maana filamu zetu zinapanda na kushuka kila siku
kwa sababu kama hio za kuridhika mapema wakati bado hatujakipata
tunachokitaka,” aliongezea.

0 comments:
Post a Comment