Baada ya kuvunjika kwa tamasha la T.I, Mei 25 kwenye ukumbi wa Irving
Plaza, New York baada mtu mmoja kufyatua risasi na kusababisha mauaji ya
mtu mmoja [Ronald MC Phatter.] na kujeruhi watu watatu, polisi
wamemkamata mtuhumiwa wa tukio hilo.
Mtuhumiwa huyo ambaye ni rapper wa Marekani anayejulikana kama Troy Ave,
anatuhumiwa kwa kufanya tukio hilo la mauaji na kujeruhi kutokana na
kamera zilizopo kwenye ukumbi.
Troy Ave, mtuhumiwa wa mauaji
Kutokana na tukio hilo lililotokea rapper T.I amepost Instagram kwa kuandika: “My
heart is heavy today. Our music is intended to save lives, like it has
mine and many others. My heartfelt condolences to the family that
suffered the loss & my prayers are with all those injured.
Respectfully, Tip.”
0 comments:
Post a Comment