Mahakama
ya Hakimu Mkazi Dodoma, jana ilimhukumu kifungo cha miaka 30, Godfrey
Mjelwa (48), baada ya kupatikana na hatia ya kuishi kinyumba na binti
yake wa kumzaa.
Hakimu
Mkazi katika mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo alisema ushahidi wa pande
zote ulithibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kuishi chumba
kimoja na binti yake, kama mke na mume.
Kwa
mujibu wa ushahidi uliotolewa, Mjelwa aliamua binti yake mwenye umri wa
miaka 15 (jina limehifadhiwa) kuwa mke na kuishi naye katika Mtaa wa
Kizota Manispaa ya Dodoma.
Hakimu Lukindo alisema kosa alilokutwa nalo mtuhumiwa ni ‘maharimu’ (kufanya mapenzi na ndugu za damu), licha ya kuwa mtoto huyo bado alikuwa mdogo, lakini ni mtoto wake wa kumzaa.
Hakimu Lukindo alisema kosa alilokutwa nalo mtuhumiwa ni ‘maharimu’ (kufanya mapenzi na ndugu za damu), licha ya kuwa mtoto huyo bado alikuwa mdogo, lakini ni mtoto wake wa kumzaa.
Mwendesha
mashtaka Janeth Mgome, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa
mtuhumiwa, ili liwe fundisho kwa wengine ambao wana tabia ya aina hiyo.
Utetezi wa mtuhumiwa huyo uliwavunja mbavu watu waliokuwapo mahakamani hapo, kwani alitaka kupunguziwa adhabu kwa kuwa mtoto wake ana miaka 14 na miezi tisa na siku tisa, siyo miaka 15 kama ilivyodaiwa mahakamani hapo.

0 comments:
Post a Comment