Chama
cha Alliance for Democratic Change ADC kimewafuta uanachama wanachama
wake wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Said Miraaj,Katibu
Mkuu Bi.Lydia Bendera,Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi Bwana Jumanne
Magafu pamoja na Katibu wa Kamati ya ulinzi Bwana Juma Wandwi kwa makosa
ya kukiuka katiba ya chama hicho kwa kususia kushiriki uchaguzi mkuu wa
marudio wa Zanzibar.
Maamuzi
hayo yamefikiwa katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo akizungumza
baada ya ufunguzi aliyekuwa mlezi wa chama cha ADC ambaye pia ni Waziri
wa Kilimo Zanzibar,Mhe.Hamad Rashid amesema katiba ya chama inasisitiza
ushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,hivyo kutoshiriki
ni kukivunja nguvu chama katika mikakati yake ya kuchukua dola.
Akizungumza
na wajumbe wa mkutano mkuu wa -ADC- Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa
Bwana Sisty Nyahoza amesema kitendo cha chama cha siasa kutoshiriki
uchaguzi kinakwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa na malengo ya
kuanzishwa chama Chochote
cha siasa na kusisitiza ipo haja ya kuangalia mfumo wa usajili wa vyama
utakaowezesha kutoa adhabu kwa vikavyoonekana kukataa kushiriki katika
chaguzi.
Aidha katika mkutano mkuu huo, wajumbe
wamemchagua aliyekuwa mlezi wa ADC ambaye kwa sasa ni Waziri wa Kilimo
Zanzibar Mhe.Hamad Rashid kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa na
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Doyo Hassan Doyo
amechaguliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu wa chama.
0 comments:
Post a Comment