Hivi ndivyo mandhari nzuri na ya kuvutia ya Daraja la
Nyerere lionekanavyo kwa juu pamoja na flai ova yetu ya kuingilia
darajani hapo ndani ya Wilaya mpya ya Kigamboni.
Sehemu ya mageti ambapo magari yanapaswa kupita wakati wa kufanya malipo yanayotarajiwa kuanza Mei Mosi 2016.
Mhandisi wa Mradi kutoka kampuni ya China Railway
Construction Engineering Group and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV)
Jamal Mruma akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari kuhusiana na ubora wa daraja
hilo.
Mhandisi Mruma alisema kuwa Daraja hilo limejengwa kwa ubora
mkubwa na lina uwezo wa kuhimili uzito zaidi ya tani 50,lakini kwa sasa
magari yanayoruhusiwa ni yale yenye tani kumi kushuka chini,"kwa sasa
tunadhibiti uzito mkubwa kwa sababu kuna baadhi ya maeneo bado
hayajakamilika ikiwemo na barabara ya kuingilia Kigamboni,ambako
hakuwezi kumudu kupitishwa uzito mkubwa",alibainisha Mhandisi Jamal.
Meneja Mradi kutoka NSSF,Mhandisi Karim Mataka
akizungumzia namna baadhi ya Madereva ambao wamekuwa wakikiuka
taratibu/sheria na alama zilizowekwa katika daraja hilo kubwa Afrika
Mashariki ambalo linatarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 100 iwapo
litapata matunzo stahiki.
Mhandisi Karimu amebainisha kuwa magari
yanayopaswa kupita hapo kwa sasa yawe chini ya tani 10,kwa sababu kwa
upande wa Kigamboni bado baadhi ya barabara hazijakamili,hivyo ni vyema
Madereva wote wakawa makini.
Daraja
hilo ambalo litaanza kutumika rasmi kwa kulipia Mei Mosi 2016,Mhandisi
Karimu amewataka Watanzania kulinda miundo mbinu ya daraja hilo ikiwemo
kutii sheria zote za Daraja hilo ili kuepuka kusababisha uharibifu wa
aina yoyote ile,kwa sababu limejengwa kwa gharama kubwa na linahitaji
matunzo.
Mhandisi
alibainisha pia kuwa Daraja hilo la Kigamboni ambalo lilizinduliwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na
kulibatiza jina la Daraja la Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF),
Moja ya Lori likikatiza darajani hapo kwa kukiuka taratibu na sheria za Daraja hilo.
Muonekano wa Daraja la Mwal Nyerere kama lionekanavyo kwa
mbaali kidogo unapoelekea kwenye mageti ya kutokea upande wa pili wa
Kigamboni.Daraja hilo limerahisisha usafiri wa kutoka Kigamboni mpaka
kati kati ya jiji la Dar.
Sehemu ya muonekano wa daraja hilo linapokatiza mkondo wa bahari
0 comments:
Post a Comment