Tuesday, April 26, 2016

UVCCM Arumeru walaani kitendo cha Mwenyekiti Mkoa kumsimamisha kamanda wao

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya

BARAZA la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Arumeru umelaani kitendo cha UVCCM mkoani hapa kumsimamisha kamanda wa umoja wa Vijana wa UVCCM wilaya ya Arumeru Mathias Manga kutokana na kuisaliti CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.


Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo

Aidda baraza hilo limelaani tamko lililotolewa wiki iliyopita na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Sabaya na kumtaka ajitathmini na kujipima kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa,kama ataona hawezi ajing'oe mwenyewe.

Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya,alisema kuwa wanamtambua Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC),kama Kamanda wao wa vijana.

"Tunalaani tamko lililotolewa na Mkoa na hatumtambui kamanda mwingine,Kamanda wetu hajatendewa haki,wajumbe wa baraza tumetathmini tamko la Lengai tunaona ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni,amepoka madaraka yasiyo yake,kitendo ambacho ni kurudisha chama nyuma badala ya kukijenga.

Mungaya alisema kuwa "Sabaya ajitathmini,ajipime kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa kwani tunaona akiendelea hivi kukiuka kanuni atakiua chama,ni bora ajing'oe mwenyewe kama anaona hawezi,tunampa siku saba akanushe madai aliyoyatoa dhidi ya kamanda wetu".

Alisema kuwa tamko hilo ni batili na hawalitambui na kumtaka Manga asivunjike moyo aendelee na haratkati za kukijenga chama hivyo asirudishwe nyuma na changamoto anazokabiliana nazo.Akizungumzia yeye kuwepo kwenye baraza hilo alidai kuwa siku ya kikao alikuwepo ila alikataa kupiga kura ya kumkataa Kamanda wake na kuamua kutoka nje.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger