Hali ya
kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara si
nzuri jambo ambalo limekuwa kero kwa abiria pamoja na watoa huduma hiyo
ya usafiri.
Kituo hicho kilichopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es
Salaam kimesheheni madibwi ya maji hivyo wadau mbalimbali wameiomba
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kutupia jicho kituo hicho na
kukifanyia ukarabati wa kumwaga kifusi kuondoa kero hiyo.
0 comments:
Post a Comment