Staa wa Filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa sababu ya
kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mwanamuziki Baraka Da Prince ni
kuhitaji penzi la kweli na si vinginevyo.
Akipiga
stori na Ijumaa, Nisha alisema kuwa watu wamekuwa wakimsengenya kwa
kudai kuwa eti yeye kuwa na Baraka ni sawa na ‘kumbemenda’ lakini
akajitetea kwamba penzi la siku hizi haliangalii umri, kikubwa ni penzi
la kweli.
“Unaweza
kuwa na mtu mzima mwenzako na msielewane lakini ukawa na ‘serengeti
boy’ mkaelewana hivyo mimi sioni tatizo kuwa naye na ninampenda hatari,”
alisema Nisha.
0 comments:
Post a Comment