Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-130 Hercules iliyoanguka.
Ramani inayoonesha eneo ambapo ndege hiyo ilipata ajali.
Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya
C-130 Hercules imeanguka usiku wa leo katika Uwanja wa Ndege wa
Jalalabad nchini Afghanistan na kuua watu 12.
Kanali wa jeshi la Marekani Brian Tribus
ameiambia AFP kwamba watano kati ya waliokufa walikuwa wanajeshi wa
Marekani, watano walikuwa raia wa kawaida na wawili walikuwa ni
Waafghan.
Msemaji wa kundi la wapiganaji la
Taliban, Zabihullah Mujahid alisema kupitia Twitter kwamba kundi hilo
lilitungua ndege hiyo, lakini mashirika ya habari yanasema hakuna ishara
inayoonesha ndege hiyo kama ilishambuliwa.
Jeshi la Marekani limesema linachunguza kilichosababisha ajali hiyo.
Ajali hiyo ya ndege imetokea huku ndege
za kijeshi za Marekani zikisaidiana na wanajeshi wa Afghanistan kujaribu
kukomboa mji wa Kunduz uliotekwa na wapiganaji wa Taliban.
Takriban wanajeshi 10,000 wa Marekani
wamo Afghanistan baada ya mpango wa kuondoa majeshi hayo asteaste
kubadilishwa mapema mwaka huu.
Rais Obama alikuwa ameahidi kuacha
wanajeshi wachache sana wa Marekani nchini humo ambao wangekuwa wa
kulinda ubalozi wa Marekani kufikia mwisho wa mwaka 2016.
0 comments:
Post a Comment