Tukio hilo lilijiri hivi karibuni majira saa 2 asubuhi maeneo ya Majengo, wilayani Misungwi, mkoani Mwanza na kujaza watu wengi.
Shuhuda wa tukio hilo aliliambia gazeti hili kuwa walisikia kelele za mtu akiomba msaada na walipotoka nje, walimuona mwanamke huyo akitoka ndani ya nyumba hiyo na kuanza kutimua mbio.
“Baada ya kumkimbiza na kumkamata, tulimuweka chini ya ulinzi na kumhoji, akashindwa kujieleza kwa usahihi, tukaamua kumuachia aende zake, lakini kuna baadhi ya watu hawakuridhika, wakaendelea kumhoji, ndipo akatoa hirizi na pasipoti za watu ambazo hakusema anazitumia kwa mambo gani,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Mama wa nyumba iliyotokea tukio hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Mama Neema, alisema asubuhi ya siku hiyo saa 1 asubuhi aliagana na mumewe aliyeelekea kazini kabla ya kufunga milango yote kwa makomeo na kulala.
Dawa alizokutwa nazo baada ya kupekuliwa.
“Nimeamka saa 2 asubuhi nikamkuta huyo bibi amekaa sebuleni, nikamuuliza
wewe ni nani? Unatafuta nini humu na umepitia wapi?, hakujibu kitu
ndipo nikatoka nje na kuanza kupiga kelele.“Wakati naendelea kupiga kelele nikakumbuka mwanangu nimemuacha ndani amelala, nikarudi maana nilihisi angemdhuru, wakati nafungua mlango yule bibi alitoka nduki hapohapo watu waliokuwa wamekusanyika nje walianza kumkimbiza.”



0 comments:
Post a Comment