Mwenyekiti wa chama cha siasa (Democratic Party - DP) nchini Tanzania, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia alfajiri ya leo katika ajali ya gari iliyotokea kwenye kijiji cha Msola mkoani Pwani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar Mohamed amethibitisha.
RPC
Mohamed amesema Mtikila alikuwa akitokea Morogoro kuelekea Dar es
Salaam na alikuwa na watu wengine watatu katika gari hilo ambao
wamejeruhiwa.Amesema chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa.
0 comments:
Post a Comment