BAADA ya kifo cha mtoto wa aliyekuwa nyota wa muziki nchini Marekani,
Whitney Houston, Kristina Brown, kutokea mapema Julai mwaka huu,
shirika la uchunguzi wa kifo hicho, The Fulton County Medical Examiner
limesema limepata majibu ya kifo hicho.
Hata hivyo, shirika hilo limesema kuwa haliwezi kuweka wazi chanzo cha kifo hicho kwa ajili ya usalama.
Awali kulikuwa na taarifa kwamba chanzo cha kifo hicho kilitokana na
kuwekewa sumu kwenye kinywaji chake huku akishutumiwa mpenzi wake, Nick
Goldon.
Kristina alikutwa ameanguka bafuni kwake mjini Atlanta ambapo ilikuwa
Januari 31 mwaka huu na kupoteza fahamu kwa miezi sita mpaka anapoteza
maisha Julai 26.
0 comments:
Post a Comment