BAADA ya kupita ukimya mrefu bila
kuzungumzia mapenzi, mrembo asiyepoteza ubora wake, Wema Sepetu ‘Madam’
amemtaja mwanaume anayetarajia kumzalia mtoto kuwa ni Luis Munana, raia
wa Namibia.
Wema
alifunguka hayo juzikati mara baada ya mwandishi wetu kutaka kujua ana
mpango gani kwenye ulimwengu wa ‘malovee’ ndipo alipomwanika Luis kuwa
ndiye mwanaume pekee ambaye ameshafikia hatua ya kumuamini na yuko
tayari kuzaa naye kwa namna yoyote licha ya kujua ana tatizo la uzazi.
“Luis
ndiyo kila kitu kwangu, ndiye mwanaume ambaye tunaelewana na siyo
mswahili kama kina mwafulani. Luis nitazaa naye hata kwa ku-adopt
(kuasili) mtoto kama njia za kawaida zitashindikana, ndiye mwanaume
ambaye nimepanga aje kuwa baba wa watoto wangu,” alisema Wema.
Kabla
ya kufunguka hayo, Wema alikuwa akimposti mwanaume huyo ambaye
alishiriki Shindano la Big Brother-Hotshorts (2014) kwenye ukurasa wake
wa Instagram pasipo kuandika kama ni mpenzi wake lakini kwa sasa ameamua
kuweka kila kitu hadharani.
Miezi
kadhaa iliyopita, Wema aliwahi kuonekana na Luis katika pati ya
Instagram iliyofanyika kwenye Viwanja vya Posta jijini Dar kisha wawili
hao kudaiwa kulala pamoja katika hoteli moja jijini humo
0 comments:
Post a Comment