KUMBUKUMBU ya
kusikitisha! Siku chache baada ya kushinda kesi ya ubakaji wa
shemejiye, Emmanuel Mbasha ameibuka na kusimulia jinsi alivyonusurika
kujitoa uhai wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiunguruma, Risasi Jumamosi linaandika.
‘Akimnong’oneza’ mwandishi wetu kwa njia
ya simu Jumatano ya wiki iliyopita katika mahojiano maalum, Mbasha
alisema kesi hiyo ilikuwa ikimuumiza moyo na kujiona hana thamani ya
kuendelea kuishi hivyo njia bora ya kuepukana na kadhia hiyo ni kujitoa
uhai.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha. |
Mbasha, ambaye alikuwa mume wa mwimbaji
wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha alisema kitendo cha jamii kuaminishwa
kuwa alitenda unyama huo, akiangalia heshima aliyonayo ikiwemo kueneza
Injili kwa njia ya uimbaji, ilikuwa ni aibu mbaya ambayo kwa ujasiri wa
kibinadamu haikuwa rahisi kukabiliana nayo.
Katika mazungumzo na mwandishi wetu,
alisema mara nyingi watu wa karibu naye wakiwemo wazee wenye busara
walishtukia njama zake za kutaka kujiua na kuamua kuwa naye karibu huku
wakimpa nasaha za kumfariji na kwamba Mungu alikuwa akimpitisha kwenye
jaribu hilo kwa makusudi maalum.
“Yaani wewe acha tu kaka, hakika
nilitaka kujiua kabisa, ni bora ningesingiziwa mambo mengine na si
kubaka, nikiangalia heshima yangu kwenye jamii, nikifikiria maisha ya
jela tena kwa kosa la kusingiziwa, kwa kweli sikuona kabisa thamani
yangu duniani,” alisema Mbasha.
TUJIKUMBUSHE
Mbasha alikuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17, kinyume cha sheria.
Katika shitaka la kwanza, Mbasha
alidaiwa kuwa Mei 23, 2014 alimbaka shemeji yake katika eneo la Tabata
Kimanga huku katika kosa la pili la kesi hiyo, akidaiwa kufanya kosa
hilohilo kwa mtu huyohuyo ndani ya gari.
Hukumu iliyomuacha huru ilitolewa
Jumatatu ya wiki hii katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala,
ambapo hakimu Flora Mujaya alisema kwa mujibu wa sheria juu ya madai
hayo, Mbasha hakuwa na hatia.
0 comments:
Post a Comment