Chama cha Mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA kupiga mawe na kutupa chupa, baadhi zikiwa na mikojo, kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga jana, tarehe 28 Septemba 2015, kabla na baada ya mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tangamano, Tanga Mjini.
Kama
ilivyo kawaida yetu miaka yote, CCM iliazimia kufanya kampeni za amani,
zinazoheshimu sheria za nchi na utu wa wapinzani wetu. Hadi sasa,
tumeweza kuwadhibiti wapenzi, washabiki na wanachama wa CCM wasifanye
vitendo vya ufunjifu wa amani.
Tukio
la Tanga sio la kwanza. Tarehe 27 Septemba 2015 viongozi wa UKAWA
waliwapanga vijana, katika eneo la stendi ya Uyole, mkoani Mbeya ili
wasimamishe msafara wa Mgombea wa Urais wa CCM na kumfanyia vurugu na
kumpigia kelele ili wananchi wasimsikie vizuri.
Ingawa Mgombea wetu alifanikiwa kukabiliana na hali hiyo, tunaamini kwamba huu sio ustaarabu. Washabiki wa CCM pia wana uwezo wa kupanga na kufanya mambo haya, tena kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Ingawa Mgombea wetu alifanikiwa kukabiliana na hali hiyo, tunaamini kwamba huu sio ustaarabu. Washabiki wa CCM pia wana uwezo wa kupanga na kufanya mambo haya, tena kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Lakini
viongozi wa CCM wa ngazi zote wamekuwa wanawahimiza wasifanye mambo
haya kwasababu CCM hatuamini kwamba hiyo ni njia sahihi ya kuomba ridhaa
ya Watanzania kuliongoza taifa letu na pia, kwa kuwa sisi ndio
tuliokabidhiwa na Watanzania nchi hii kuiongoza, tunafahamu dhamana yetu
kubwa ya uongozi wa taifa na ulinzi wa amani ya Taifa letu.
Tunawasihi
wenzetu wa UKAWA kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni kilichobaki,
tufanye kampeni kwa amani ili tumalize uchaguzi kwa amani na taifa
liendelee kuwa na amani baada ya uchaguzi.
Wenzetu
wa UKAWA wasitufikishe mahala ambapo washabiki wa CCM watashindwa
kuvumilia kuona Chama chao na viongozi wao wanadhalilishwa.
Tukio la Tanga la Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kupigwa mawe limewaudhi na kuwakera wana-CCM na wapenda amani wote wa Tanga.
Hata
hivyo, tumewasihi wana-CCM wasilipize kisasi. Chama chetu kina dhamana
ya uongozi wa nchi na ulinzi wa amani ya nchi yetu. Wenzetu dhamana hiyo
hawana.
Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa.
Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa.
Tunawapongeza wana-CCM kote nchini kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni.
Tunawashukuru kwa kubaini na kutoyumbishwa na propaganda za wenzetu ikiwemo ya Tanga, kwamba mkutano wa Tanga uliahirishwa kwasababu watu walikuwa wengi.
Tunawashukuru kwa kubaini na kutoyumbishwa na propaganda za wenzetu ikiwemo ya Tanga, kwamba mkutano wa Tanga uliahirishwa kwasababu watu walikuwa wengi.
Itakuwa
ni mara ya kwanza katika historia kwamba mkutano wa kampeni
unaahirishwa kwasababu ya wingi wa watu. Katika mikutano ya kampeni,
ikiwemo ya CCM, na hata katika sherehe za kitaifa, baadhi ya watu
huzidiwa nguvu na huhudumiwa na wahudumu wa huduma ya kwanza huku
mikutano ikiendelea.
Hii
haitakuwa mara ya kwanza kwa wenzetu kutafuta kisingizio cha kutofanya
mikutano ya kampeni. Mkutano wa kampeni ya UKAWA wa Geita pia
waliuahirisha kwa kisingizio tofauti, kwamba jukwaa na vipaza sauti
havikuandaliwa ingawa aliyetangaza kuahirisha alisimama jukwaani na
akasikika na watu wote.
Mabadiliko
wanayoyahubiri wenzetu yanaanza na kusema ukweli. Imefika mahali sasa
wenzetu wa UKAWA wawaeleze ukweli Watanzania kuhusu mgombea wao
kushindwa kuhutubia baadhi ya mikutano au kuhutubia kwa dakika 3 kuliko
kuwahadaa kwa kutengeneza matukio na vioja ili kuficha mapungufu ya
mgombea wao.
Tunarudia
kuwataka viongozi wa UKAWA kuacha kupanga vurugu, kuharibu mali za CCM,
na kutukana wana-CCM. Tunarudia kuwataka waache kauli zao za kuibiwa
kura.
Kauli hizo ni za kukata tamaa na kuwandaa watu kufanya fujo. Tunadi sera zetu na wagombea wetu kwa amani ili tuwape Watanzania fursa ya kuchagua kwa amani ili taifa liendelee kuwa la amani, umoja, utulivu na mshikamano mara baada ya uchaguzi.

Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
29.09.2015
0 comments:
Post a Comment