Thursday, July 23, 2015

Umri wa kuoana nchini hispania waongezwa kutoka miaka 14, sasa ni miaka 16 kulingana na sheria za nchi

Umri wa kuoana nchini Uhispania sasa ni miaka 16 kulingana na sheria ya nchi
Uhispania imeongeza umri wa ndoa kutoka miaka 14 hadi 16 , ikiwa ni nchi iliyoidhinisha umri wa chini zaidi wa kuolewa barani Ulaya.
Kabla ya kupandishwa kwa miaka, wavulana na wasichana wangeweza kuolewa wakiwa na miaka 14 kwa ruhusa ya hakimu.
Mashirika yanayotetea haki za watoto yameafiki kuongezwa kwa wa kuolewa Uhispania
Mabadiliko hayo yamekuja miezi kadhaa baada ya serikali kuongeza miaka ya idhini ya kuolewa kutoka miaka 13 hadi 16.
Serikali ilitangaza azma yake ya kufanya marekebisho ya sheria mwezi Aprili 2013, lakini mabadiliko hayo yameanza kutekelezwa leo Alhamisi.
Uhispania limekua ni taifa lenye sheria inayoruhusu ndoa ya umri mdogo zaidi barani Ulaya
Hatua hiyo imeafikiwa na maafisa kutoka shirika la watoto duniani Unicef na makundi ya haki za watoto nchini Uhispania.
Kwa mujibu wa gazeti la El Pais (nchini Uhispania), ni ndoa 365 zilizowahusisha wavulana na wasichana wa chini ya miaka 16 zilizofungwa kati ya mwaka 2000 na 2014 - huku tano tu zikifungwa mwaka 2014.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger