Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilakiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrer Mngereza alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
Marehemu Banza Stone, aliyefariki jana mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu, amezikwa jioni hii katika makaburi ya Sinza. Marehemu Banza Stone atakumbukwa kwa umahiri wake wa utunzi na uimbaji alipokuwa na bendi mbalimbali zikiwemo Twanga Pepeta, Tot na Extra Bongo.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Ramadhani Masanja "Banza Stone" likitolewa nyumbani tayari kwa mazishi Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
0 comments:
Post a Comment