Aliyekuwa mume wa mwanamuziki wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha.
Mwisho wa reli? Aliyekuwa mume wa mwanamuziki wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameapa kwa kulamba kidole, kukichovya kwenye mchanga kisha kukipitisha shingoni kuwa, hana mpango wa kurudiana na mkewe huyo katika maisha yake.
Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, Mbasha aliweka wazi maumivu aliyokuwa akiyapitia wakati akiwa kwenye ndoa na Flora hivyo ameona njia bora ya kujipatia furaha ni kumuacha aishi maisha yake na yeye afanye yake.
Mbasha alikiri kufanya jitihada za ziada akiwatumia ndugu, jamaa na marafiki kumshawishi Flora kurejesha upya penzi lao, lakini amekuwa akiambulia maneno makali na matusi.
“Mimi na Flora basi tena, acha ibaki historia, amenitesa sana kihisia,” alisema Mbasha.
0 comments:
Post a Comment