Friday, April 5, 2013

NATONGOZWA SANA FACEBOOK MPAKA BASI-CHUCHU HANS

Msanii wa filamu Bongo ambaye ni mke wa mtu, Chuchu Hans amefunguka kuwa  anatongozwa sana na wanaume kupitia Mtandao wa Kijamii wa Facebook, kitendo kinachomkosesha amani.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Chuchu alisema kuwa, anachojua yeye mtandao huo ni sehemu ya kukutana na marafiki na kubadilisha mawazo lakini cha ajabu kila akiingia, wanaume kibao wamekuwa wakimtaka.
“Mimi kwa kweli kila nikiingia Facebook nakutana na wanaume ambao wananitongoza, mtu anajua kabisa una mtu wako lakini bila haya anatangaza dau na kueleza kuwa, anakutaka, mijitu hii naichukia kweli,” alisema Chuchu
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger