BAADA ya kupiga shoo pande za Afrika Kusini, mwanadafada anayekimbiza kwenye anga la muziki wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema amejifunza mambo mengi kupitia ziara hiyo.Akipiga stori na Stori 3 juzikati baada ya kurejea Bongo, Shilole alisema kwanza amejitambua na kupata mbinu mpya za kuhimili jukwaa hata kwa watu wasioelewa lugha unayoimba, mbinu mbalimbali za kujitangaza na ushirikiano.
“Nimejifunza mambo mengi, muziki una nguvu kubwa watu wanakuelewa kama una mbinu za kuwashawishi unapokuwa jukwaani, mashabiki wangu waendelee kunipa sapoti kwani mambo ndiyo kwanza yameanza,” alisema Shilole.
0 comments:
Post a Comment