Monday, March 4, 2013

Kuelekea Uchaguzi Nchini Kenya,Kituo cha polisi chashambuliwa mjini Mombasa na polisi kadhaa kuuawa

Takriban polisi wanne mjini Mombasa, Kenya, waliokuwa wamesambazwa kuhakikisha amani kwenye uchaguzi wa urais unaofanyika leo wamevamiwa na kuuawa na kundi la watu saa chache kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa.
kenyavote1.jpg.size.xxlarge.letterbox
Kwa mujibu wa BBC washambuliaji waliokivamia kituo cha polisi mjini Mombasa wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Pwani la Mombasa Republican Army (MRC) ambao wamekuwa wakipigania uhuru wa jimbo la Pwani.
Hata hivyo shambulizi hilo huenda halihusiani na masuala ya uchaguzi.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger