Showing posts with label wasa. Show all posts
Showing posts with label wasa. Show all posts

Friday, November 8, 2013

THEA WA BONGO MUVI AACHANA NA MUMEWE MARA BAADA YA KUBAINI KUWA MUMEWE NI KICHECHE..!!

NDOA ya mastaa wa filamu, Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ imevurugika baada ya kutokea hali ya kuzinguana kwa wawili hao chanzo kikidaiwa ni kukosekana uaminifu.
Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ siku ya ndoa yao.
 
Chanzo cha habari hii ambacho ni rafiki wa Thea kilieleza kuwa, kutibuana kwa wanandoa hao kumekua kufuatia Thea kuhisi mwenzake anamzunguka.“Kimsingi hali si shwari, ndoa inawaka moto, Thea anamtuhumu Mike kuwa anamsaliti, chanzo ni hizi simu na siku hiyo mtiti ulipotokea, shosti alikwenda kwao na mpaka leo hii (Juzi Jumatato) anasubiri wasuluhishwe,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, Mike alitafutwa na alipoulizwa kuhusu ndoa yake kutibuka alisema: “Mh! Watu ni wambeya sana mimi na mke wangu tulitokea kutoelewana na si mambo ya meseji wala wanawake, mimi sina mambo hayo kabisa, siwezi kuongelea mambo mengi mpaka nitakapoenda nyumbani kwa mke wangu lakini kilichotokea ni cha kawaida tu .”Thea hakuweza kupatika kuzungumzia ishu hiyo.
Share:

Sunday, May 19, 2013

MR. NICE AURUDIA TENA "UKICHECHE" ULIOMFANYA AFILISIKE


Hakika  Tabia  ni  ngozi....
Ni vigumu  kuamini, lakini  ukweli  ni  kwamba Mr.Nice  ameirudia  tena  ile  tabia  yake  ya Ukicheche  na  kuwapanga  wanawake  mithiri  ya vyombo  kabatini  iliyomfanya  afulie  na  hatimaye  kuwa  omba omba.....
Taarifa  toka  nchini Kenya  ambako kwa  sasa  msanii huyo  yupo huko  ni  kwamba, Mr. Nice   kwa  sasa   alala  baa  akiwa  amezungukwa  na  warembo  kadhaa wanaojua  kuzitumia  pesa...!!!!

Nice amekuwa  akionekana  katika  mitaa kadhaa  ya jiji  la Nairobi akiwa  na  "mabodigadi wa kike" ambao  amejitolea  kuwadhamini   LUNCH, DINNER na MATANUZI  mengine...
Hongera  kwa  moyo wa upendo Mr. Nice...Tunajua  kwamba  si  vizuri  tukakupangia  matumizi  ya pesa  yako, lakini  tunakuonea  huruma  maana  historia  yako  tunaijua tangu  enzi  zile  ulipokuwa   ukitamba  na  nyimbo  zako  za "Kikulacho  ki  nguoni  mwako"   kabla  ya  kufilisiwa  na  akina  dada  wa  mjini....
Share:

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger