Monday, May 2, 2016

SUMATRA:Daladala Kuanza Kupitisha Abiria Daraja la Kigamboni

April 16 2016 ni siku ambayo wakazi wa kigamboni walianza kulitumia daraja la ‘Nyerere’ Kigamboni na baaadae Daraja la Nyerere ‘kigamboni’ lilifunguliwa rasmi April 19 2016 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John pombe Magufuli.

Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) David Mziray ameongelea uanzishwaji wa usafirishaji wa abiria kwa daladala kupitia daraja la Nyerere ‘Kigamboni’ Dar es salaam.

Tunaomba kuhamasisha wamiliki wa mabasi kuja kupata leseni kwa ajili ya kutoa huduma ya Kigamboni kwenda mbagala rangitatu, kigamboni kwenda temeke, kigamboni- stesheni, sasa hivi njia hizo ziko wazi, tunahamasisha magari ambayo yanabeba abiria 27 na kuendelea, nauli zinaanzia 400 mpaka 450
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger