WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeamua kupambana na wala rushwa
ili kiasi kidogo cha rasilmali kilicholengwa kiweze kuwafikia wananchi.
Ametoa
kauli hiyo juzi (Jumamosi, Mei 14, 2016) wakati akizungumza na
Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi
wa Tanzania jijini London, Uingereza.
“Jambo
tuliloamua kuanza nalo ni kupambana na rushwa. Tumeamua kufanya hivyo
ili kurudisha umoja na maelewano miongoni mwa Watanzania, tunataka
tuibadili Tanzania ili iwe ni ya Watanzania wote… tumechoka kuambiwa
sehemu fulani mradi umekamilika halafu ukienda kuangalia hukuti kitu na
fedha ile haipo,” alisema huku akishangiliwa.
Akizungumzia zoezi la kusaka watumishi hewa, Waziri Mkuu alisema Serikali itawashughulikia wale wote waliohusika na zoezi hilo.
“Wafanyakazi hewa wamefikia zaidi ya 10,000 na tumeokoa zaidi ya sh. bilioni 4.5 zilizokuwa zikipotea kila mwezi. Tukikamilisha zoezi la kusaka watumishi hewa, sasa tutataka kujua ni akina nani walikuwa wakipokea fedha hizo. Waliohusika tutashughulika nao,” alisisitiza.
“Wafanyakazi hewa wamefikia zaidi ya 10,000 na tumeokoa zaidi ya sh. bilioni 4.5 zilizokuwa zikipotea kila mwezi. Tukikamilisha zoezi la kusaka watumishi hewa, sasa tutataka kujua ni akina nani walikuwa wakipokea fedha hizo. Waliohusika tutashughulika nao,” alisisitiza.
Alisema
hivi sasa Serikali inalenga kuwa na watumishi ambao wanafanya kazi kwa
uaminifu, uadilifu na uwajibikaji mahali pa kazi. “Hiki ndicho kipaumbele cha Serikali ya awamu ya tano na tena zoezi hili litakuwa endelevu”, alisema Waziri Mkuu.
Akizungumzia
kuhusu ukuaji wa uchumi, Waziri Mkuu ambaye alikuwa London kuhudhuria
mkutano uliojadili mapambano dhidi ya rushwa kwa niaba ya Rais Dk. John
Pombe Magufuli, alisema lengo la Serikali hivi sasa ni kuona kuna ukuaji
wa uchumi unaoenda sambamba na huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Alisema
viwanda vingi viliuzwa na watu waliovinunua wakageuza kuwa ni maghala
ya kufugia wanyama. Sisi tunataka vifufuliwe ili teknolojia mpya na za
kisasa zije Tanzania. Nafasi ya kuwekeza iko kwa Watanzania wote walioko
nyumbani na ninyi mlioko nje,” alisema.
Alisema
ardhi ipo ya kutosha na akawataka wawaalike marafiki zao waje kuwekeza
nchini, ili mradi wawe ni watu makini, wenye nia ya dhati ya kuwekeza
nchini na wenye mitaji na siyo madalali (middlemen).
“Tunataka usindikaji wa mazao na bidhaa ufanyike nchini mwetu badala ya kupeleka mazao ghafi nje ya nchi, kwa njia hiyo tutakuwa pia tumezalisha ajira kwa watu wetu,” alisema.
“Tunataka usindikaji wa mazao na bidhaa ufanyike nchini mwetu badala ya kupeleka mazao ghafi nje ya nchi, kwa njia hiyo tutakuwa pia tumezalisha ajira kwa watu wetu,” alisema.
“Kuna
Watanzania wanaishi Botswana, Ujerumani na Poland wameshaleta
wawekezaji nchini. Kwa mfano wa Poland wameleta mradi wa umeme katika
vijiji vitani wilayani Ileje. Kwa hiyo ninyi endeleeni kuishi Uingereza
lakini mhakikishe kuwa ukaaji wenu hapa, unaleta tija kule nyumbani.
Kumbukeni Tanzania na muwe tayari kuihudumia Tanzania,” alisema.
“Serikali
inaamini itanufaika na uwepo wenu hapa Uingereza. Muweke kipaumbele cha
kuwekeza nyumbani na mkishindwa mtutafutie marafiki zenu. Mwenye uwezo
andaa andiko la mradi halafu uwasiliane na Balozi ili akusaidie kutafuta
wahusika kule nyumbani,” aliwaasa.
Akijibu
swali kuwa ana maoni gani juu ya Bunge kutorushwa ‘LIVE’, Waziri Mkuu
alisema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuwawezesha watu kufanya kazi kama
ambavyo kaulimbiu ya Mhe. Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu inavyosema.
“Bunge
la Tanzania lilikuwa ni bunge pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
na duniani ambalo lilikuwa likirushwa LIVE kuanzia asubuhi hadi usiku.
Ina maana katika kipindi cha Bunge la bajeti, ambalo linaendeshwa kila
siku kwa miezi mitatu, Watanzania nao wangekuwa LIVE kwa miezi mitatu,” alisema.
“Tulilazimika kujifunza kutoka kwenye mabunge mengine. Hivi hapa Uingereza mnaangalia Bunge live kila siku?” alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa kuwa linarushwa LIVE kwa kipindi kisichozidi dakika 15 wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu tu.
Akitoa
ufafanuzi, aliwaeleza kwamba Bunge la Tanzania linarusha ‘LIVE’ kila
siku asubuhi wakati wa maswali ya kawaida na Alhamisi asubuhi wakati wa
maswali kwa Waziri Mkuu lakini mijadala yote hurekodiwa na kuhaririwa na
kisha kurushwa kuanzia saa 8-9 mchana na saa 3-4 usiku kwa siku husika.
Kwa Watanzania wanaopenda kufanya kazi na wanapenda kufuatilia mambo ya Bungeni, walikuwa hawaoni LIVE coverage kwa
sababu walikuwa kazini lakini sasa hivi wanaweza kufuatilia masuala ya
bunge kwani muda wa jioni uliopangwa mtu anakuwa ametoka kazini na
anaweza kuangalia televisheni akiwa nyumbani baada ya kutoka kazini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, MEI 15, 2016
0 comments:
Post a Comment