Viongozi wakuu wote wa Taifa wako nje ya nchi katika ziara za kiserikali kwenye mataifa tofauti.
Rais
John Magufuli aliwasili Uganda jana asubuhi kuhudhuria sherehe za
kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Yoweri Museveni zinazofanyika
leo na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan alikuwa Kigali, Rwanda
kuhudhuria mkutano wa dunia wa uchumi.
Taarifa
zilizopatikana na kuthibitishwa na Mwandishi wa Makamu wa Rais, Penzi
Nyamngumi zimesema, Makamu wa Rais aliondoka nchini Jumanne akitokea
Dodoma na angerejea kesho baada ya mkutano huo.
Kiongozi
anayefuatia kwa wadhifa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisafiri juzi
kwenda London, Uingereza kumwakilisha Rais Magufuli katika mkutano wa
wakuu wa nchi kujadili mapambano dhidi ya rushwa.
Majaliwa katika ziara hiyo ameongozana na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, George Masaju alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya
anayepaswa kukaimu urais, alisema Makamu wa Rais amekwisha rejea nchini
na yuko Mwanza.
Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 37 (3), inaeleza kuwa
endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shughuli
za Rais zitatekelezwa na Makamu wa Rais, kama naye hayupo, yatatekelezwa
na Waziri Mkuu.
Hata
hivyo, Ibara ya 37 (6) (b) inasema Rais hatahesabiwa kwamba hayupo
iwapo atakuwa nje ya Jamhuri ya Muungano kwa kipindi cha saa 24.
0 comments:
Post a Comment