Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wiki hii
anatarajiwa kuanza kuvaa viatu vya Rais John Magufuli bungeni.
Kesho Profesa Mbarawa anatarajiwa kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Mbunge
huyo wa kuteuliwa atakuwa na jukumu kubwa la kuwasilisha bajeti hiyo
ambayo kwa takriban miaka 10 ilikuwa jukumu la Dk Magufuli.
Magufuli
alikuwa Waziri wa Ujenzi kwa miaka mingi kabla ya kujitosa kuwania
urais kupitia CCM ambako aliteuliwa na kushinda Uchaguzi Mkuu, Oktoba
mwaka jana.
Sekta
tatu alizopewa Profesa Mbarawa ni nyeti na ngumu, hivyo Watanzania
wanasubiri kuona atakavyoanza bajeti yake ya kwanza kesho tangu
kuteuliwa na Dk Magufuli kushika nafasi hiyo.
Ujenzi
bado ni sekta inayotegemewa na Taifa katika kuingiza mapato na pia
kusaidia huduma za jamii. Masuala ya ujenzi wa barabara, madaraja,
mawasiliano na uchukuzi vyote ni muhimu kwa uchumi. Hayo yanatiwa nguvu
na jitihada za Rais Magufuli za kukusanya mapato tangu aingie
madarakani.
Suala
la bandari ni eneo mojawapo litakalogusa bajeti ya Profesa Mbarawa.
Kuliibuka masuala mengi ya ufisadi katika bandari ya Dar es Salaam,
mambo yanayotegemewa kuligusa Bunge.
Mbali ya hayo, masuala ya mawasiliano yatakuwa pia na nafasi katika bajeti ya Profesa Mbarawa.
0 comments:
Post a Comment