MKAZI
wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
Julietha Sokoine (24) ambaye amejifungua watoto wa watatu na ameiomba
serikali, taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha
utakaomsaidia kuwatunza watoto hao.
Pia alisema msaada huo pia utamuwezesha kupata tiba ya ugonjwa wa pumu ambao umemsababisha kuvimba mwili wote.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, Sokoine ameiomba jamii kumsaidia kutokana na kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu ambao pia umesababishia kuwa na hali ngumu ya kimaisha ambayo inayomfanya kushindwa kuwatunza vizuri watoto wake hao.
Alisema watoto hao, Daniel Sokoine,David Sokoine na Davis Sokoine walizaliwa kwa pamoja Machi 22, mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Dodoma huku kati ya wawili wa wakiwa na uzito kilo mbili na nusu na wa mwisho kilo mbili.
“Hali yangu siyo mzuri kutokana na mimi mwenyewe kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu,ambao pia wakati mwingine ninalazimika kuwanywesha maziwa ya ngombe watoto hao pindi ninapozidiwa na ugonjwa huo”alisema .
Kwa upande wake baba wa watoto hao Sokoine Chipanta alisema pamoja na juhudi nilizofanya za kilimo hata hivyo mazao yalinyauka na jua.
Alisema kutokana na hali hiyo analazimika kutafuta vibarua ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kununua chakula pamoja na matunzo ya watoto hao.
Alisema kwa wale wote watakaoguswa na kuamua kumpa msaada wawasiliane naye kwa namba ya simu +255 652 744 510.

0 comments:
Post a Comment