Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema idadi ya namba tambulishi
ambazo zilikuwa hazina viwango zimeendelea kupungua kutoka asilimia 30
mwezi Desemba hadi kufikia asilimia 13, Machi mwaka huu.
Kutokana na kupungua huko, inamaanisha kwamba simu feki nchini zinazidi kupungua.
Akizungumza na vyombo vya habari jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TCRA James Kiraba amesema katika uchambuzi na matokeo ya awali ambacho
pia kilishirikisha kampuni za mawasiliano kimeonyesha kuwa mwezi
Februari ilishuka mpaka asilimia 18.
Amesema uchambuzi wa Februari ulionyesha idadi ya namba tambulishi
ambazo hazikuwa na viwango zilikuwa asilimia tatu, vilevile idadi ya
namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa na asilimia 18, huku simu
halisi zikiwa asilimia 79.
“Uchambuzi wa Machi unaonyesha idadi ya namba tambulishi ambazo
hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia nne, huku idadi ya namba
tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa asilimia 13. Uchambuzi huu
unahusisha kampuni zote za simu nchini,” amesema Kiraba.
Source: Mwananchi

0 comments:
Post a Comment