Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini jijini Dar es Salaam na kuipongeza Serikali kwa kufanikisha ujenzi huo.
Mama Maria Nyerere aliyeongozana na mwanaye, Makongoro Nyerere amesema kukamilika kwa daraja hilo, ambalo ujenzi wake umegharimu Sh254.12 bilioni, kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Mwalimu Julius Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja hilo lakini akakwamishwa na ufinyu wa bajeti.
Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuamua liitwe Daraja la Nyerere kwa heshimu ya Baba wa Taifa na amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo kutambua juhudi zilizofanywa na mmewe katika ujenzi wa nchi.
"Ninamshukuru sana Rais kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini Mungu akamjalia akasema kwamba hapana tukumbuke tulikotoka. Kwa hiyo najisikia vizuri sana na familia nayo inajisikia vizuri sana,” alisema.
Mama Maria alisema Watanzania wanajisikia vizuri sana kwa maana watakuwa wanaulizana, "Nyerere alikuwa ni nani?".
Daraja la Nyerere lenye urefu wa meta 680, upana wa meta 3.2, njia sita za magari na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais Magufuli Aprili 19, 2016.

0 comments:
Post a Comment