![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgIbTNZKMjKfs2a_eo_p5huGCGdxgjOkSBPyCSDRHnhl3xm_Snv8pTbuZjhtorag4MjeYhUPRPVh0zx3Gz7LUDF70LIdqnyBoyFbJShDekbcQfeb7cm-Hp1LFq3OTyMrPfCaKSU6SNvSNI/s640/Gwajima.jpg)
Askofu
Josephat Gwajima amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa kuwa alishiriki kama ‘mshenga’
kumshawishi mwanasiasa huyo kumpokea Edward Lowassa katika chama hicho.
Jana,
Dk. Slaa alimtaja Askofu Gwajima kama mshenga na kwamba alimshawishi
ampokee Lowassa huku akidai kuwa askofu huyo alimtamkia kuwa maaskofu 30
wa Kanisa Katoliki walihongwa na timu ya Lowassa.
Askofu
Gwajima amekanusha taarifa zilizotolewa na Dk. Slaa ambaye alikuwa
rafiki yake kwa muda mrefu akidai kuwa ni muongo mkubwa. Alisema kuwa
Dk. Slaa ameamua kuwashambulia maaskofu hao kwa kuwa anafahamu hawana
majukwaa ya kumjibu kama ilivyo kwa wanasiasa.
Gwajima alidai kuwa yeye aliitwa kama msuluhishi ndani ya Chadema na sio mshenga wa kumleta Edward Lowassa.
“Kwa
kawaida inashangaza kwamba kama watu wawili wanagombana inatakiwa awepo
mtu wa kuwaunganisha, ila anaposema maaskofu 34 haileti maana, haiingii
akili, ameingiza Gwajima, Rostam Aziz na maaskfu,” Gwajima ameliambia
gazeti la Mtanzania na kuongeza kuwa Dk. Slaa ametumwa na watu
anaowafanyia kazi.
Askofu
huyo alidai kuwa alichokisema jana Dk. Slaa kilikuwa silaha pekee ya
CCM iliyokuwa imebaki na kuwataka waumini wake na watanzania kutoamini
alichosema mwanasiasa huyo.
“Nafikiri Slaa ndio risasi ya mwisho ya mwisho iliyokuwa imebaki kwenye bunduki ya CCM,” alisema.
Juzi
Dk. Slaa alitangaza kustaafu siasa za vyama akieleza kutokana na
kutoridhishwa na mwenendo wa siasa nchini hususani Chadema aliyoijenga
kwa ajenda ya kupinga ufisadi na badala yake wamemkumbatia Lowassa
waliyekuwa wanamtuhumu kuwa fisadi mkubwa.
0 comments:
Post a Comment