LICHA ya Ubalozi wa
Marekani jijini Nairobi kusisitiza kuwa Rais Barack Obama hatatembelea
Kijiji cha K’Ogelo, alikozaliwa baba yake mzazi, bibi yake, Mama Sarah
Obama amesema atamuandalia chakula kizuri cha kiasili ukiwamo ugali na
mboga za majani za kienyeji.
Bibi huyo, mke wa tatu wa babu yake
Obama, aliwaambia waandishi kuwa anategemea kukutana na mjukuu wake huyo
kijijini K’Ogelo wakati wa ziara hiyo kwa vile anampenda na angefurahi
kutembelea kaburi la baba yake mzazi.
“Hii ndio boma ya baba yake, sasa mimi
naweza kusema nini, hakuna maneno mimi iko nayo, wewe ulikuwa nataka
mimi nachinja nini? Yeye nakula hata Omena hata mboga, chakula ile mimi
nakula ndio yeye nakula,” mama Sarah aliiambia BBC.
Kaburi la baba yake Rais Obama
limekarabatiwa kuelekea ziara hiyo licha ya Balozi wa Marekani nchini
Kenya, Robert Godec kusisitiza kuwa kiongozi huyo mwenye mvuto hatazuru
K’Ogelo.
0 comments:
Post a Comment