Chombo cha Sheria na Haki Ufilipino ilitoa amri siku ya Jumanne usiku kumzuia Chris Brown kuondoka nchini humo mpaka atakapolipa hela za Promoters walioandaa show kipindi cha mwaka mpya, show ambayo Chris hakutokea.
Kwa sasa Chris Brown ameambiwa kama atahitaji kuondoka nchini humo kwa sababu za msingi basi itambidi aombe ruhusa kwa Ofisi ya Uhamiaji ambao kama wakikubali basi watampatia cheti kinachoonyesha sababu hizo ni za mzingi na kuwa atarudi.
0 comments:
Post a Comment