
Kenya imekua nchi yenye rekodi ya matukio kila kukipambazuka.
Ni juzi tu kontena limekamatwa bandarini Mombasa likiwa na vikaragosi vya mafuvu ya watu pamoja na mifupa ya binadamu.
October 11 2013 zimetoka stori nyingine mbili ambazo zimechukua headlines ambapo ya kwanza ni Mwanamke mwizi wa kuku kulazimishwa kula kuku mbichi baada ya kukamatwa.
Tukio jingine ni kuhusu Askari wa usalama barabarani, siku zote imezoeleka na wengi kwamba askari sio rafiki wa raia na huwa wana lugha za kijeshi.
Sasa basi, Askari kadhaa wa usalama barabarani wametoa kituko cha karne pale walipochukua Biblia na kuanza kuhubiri pamoja na kuimba nyimbo za Mungu wakiwa na sare zao hivyohivyo kuwahubiria Madereva kufata sheria za barabarani, hii ni baada ya kuona Madereva wamekua wagumu kuelewa.
Cheki video Hapa chini...
0 comments:
Post a Comment