Wednesday, February 27, 2013

"SINA NGOMA KAMA WATU WANAVYOHISI, MAZOEZI NDIO YANAYONIKONDESHA" RAY AFUNGUKA KUHUSU MKONGOROKO WA AFYA YAKE...!!

Picha hiyo ya juu inamuonesha alivyokuwa mwanzo (kushoto) na jinsi alivyo sasa (kulia).
------------
Muigizaji aliyepo kwenye list A ya waigizaji wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi aka Ray ameamua kuzungumza baada ya watu kuanza kumzushia anaumwa kutokana na kupungua mwili wake kwa kiasi kikubwa.



Ray amezikanusha tetesi hizo zilizoanza kusambaa kwa haraka ambapo gazeti la udaku la Kiu wiki hii lilikuwa na habari isemayo, ‘Ray apukutika mwili’ – Kitambi chote kwishnei! Ukimuona unaweza kumpita bila kumtambua, maombi ya wakatoliki yahusishwa.

Hata hivyo Ray amesema hali hiyo imetokana na kufanya mazoezi zaidi siku za hivi karibuni. “Jamani kwani unene ndio afya au kupungua ndio ugonjwa,” ameuliza Ray.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger