Friday, February 15, 2013

LINAH NDANI YA PENZI JIPYA...



KIJANA aliyejipatia umaarufu kwa kumvamia msukuma kambumbu wa Real Madrid, ‘Kaka’, Nagari Kombo amedaiwa kuwa ndiye anayemiliki penzi la Mbongo Fleva, Estalina Sanga ‘Linnah

Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wamekuwa wakionekana kwenye viwanja tofauti vya starehe na mara kwa mara wamekuwa wakishea vitu vyao ikiwamo gari la Linnah.
“Mbona siyo siri, Linnah na Nagari ni wapenzi kitambo na siku hizi wanajiachia bila kificho kwa raha zao. Hawamuogopi mtu,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Paparazi wetu alipomtafuta Linnah kuhusiana na ishu hiyo, alipokea simu na alipoulizwa kinachoendelea baina yao alikata simu fasta na kuizima kabisa.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger