Rais wa Marekani, Barack Obama ametoa amri kwa bendera za Marekani
kupepea nusu mlingoti kwa heshima ya kuwakumbuka waathirika waliouwawa
katika shambulizi baya la watu wengi kuliko yote katika historia ya
Marekani.
Mtu mmoja mwenye silaha aliua watu wapatao 50 na kujeruhi 53 wengine
ndani ya klabu ya usiku ambayo hutumiwa zaidi na mashoga huko Orlando
Florida Jumapili alfajiri.
Obama alitangaza kuwa kicho ni kitendo cha kigaidi na kusema FBI
wanaongoza uchunguzi. Amesema juhudi zote zinafanyika kujua nini
kilimchochea muuaji huyo kufanya hivyo au kama alikuwa na ushirikiano
wowote na makundi ya kigaidi.
Rais aliyekuwa amesikitishwa sana alilihutubia taifa lililopigwa na
butwaa kutokea White House akisema ni rahisi kwa mtu kupata silaha
kuwapiga watu mashuleni, makanisani, kwenye majumba ya sinema na klabu
za usiku.
Mwanasheria mkuu Loretta Lynch na waziri wa usalama wa ndani
Jeh Johnson wote waliahirisha safari zao kwenda Beijing kwa mazungumzo
juu ya usalama wa mitandao na maafisa wa China.
0 comments:
Post a Comment