
JESHI
la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 14 wakiwamo wanawake
wawili na mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwika
wilayani Moshi, kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha.
Miongoni
mwa watuhumiwa hao wapo wanaodaiwa kuwa majambazi sugu 10, waganga wa
kienyeji wawili ambao walikuwa wakitumika kwa ajili ya kuwapa dawa
watuhumiwa hao ili wasikamatwe na polisi na kuzindika silaha zilizokuwa
zikitumika katika ujambazi na wanawake wapishi wa watuhumiwa hao wakiwa
mafichoni.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mtafungwa alisema jana kuwa
watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Tanga na
Kilimanjaro kufuatia msako mkali wa askari uliotokana na taarifa za
siri.
Mtafungwa
alisema mwanafunzi wa sekondari ya Mwika, Kelvin Shayo (17) miongoni
mwa matukio anayotuhumiwa kushiriki ni pamoja na la kumpora bastola
yenye namba YP0466 Tz Car aina ya brown, askari mstaafu wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Elibariki Urio (67).
Kamanda
alisema silaha hiyo iliporwa Februari 25 mwaka huu baada ya majambazi
kumvamia nyumbani kwake na kupora mali pamoja na silaha hiyo kisha
kwenda kuificha nyumbani kwa Eleutery Nguma (62) mkazi wa Makami Chini,
Tarafa ya Vunjo ikiwa imefukiwa ardhini kwenye mfuko wa plastiki.
Aidha,
Mtafungwa alisema kwa mujibu wa kumbukumbu za polisi mtuhumiwa huyo
(Nguma) ilidhaniwa kuwa ameacha vitendo vya ujambazi lakini amebainika
kuwa ni mpangaji wa njama za ujambazi, kuficha mali za wizi pamoja na
kuficha silaha zinazotumika katika uhalifu.
0 comments:
Post a Comment