RAIS John Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurungezi wa Kituo cha
Uwekezaji (TIC) Juliet Kairuki kwa kile alichokiita “Julieth Kairuki
amekua hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa mwezi Aprili
2013,
Taarifa iliyotolewa leo na Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, inasema utenguzi huo umefanyika tangu tarehe 24, Aprili mwaka hu na kwamba kitendo cha Kairuki kutochukua mshahara wake kinazua maswali mengi.
Hata hivyo taarifa hiyo inasema endapo Kairuki atakuwa tayari kufanya kazi na serikali atapangiwa kazi nyingine.
Kairuki aliteuliwa tarehe 12 Aprili, 2013 na Rais wa awamu ya nne,
Jakaya Kikwete kushika nafasi hiyo iliyoachwa na mtangulizi wake Ole
Naiko kustaafu.
Kabala ya kuteuliwa kuongoiza kituo hicho Kairuki alikuwa Meneja Mkuu
wa Idara ya Benki na Huduma za Fedha katika Chama Cha Mabeki Afrika
Kusini.
Taarifa zilizo wahi kuandikwa na gazati la MAWIO lililofutwa na
serikali , zinasema tangu Kairuki aajiriwe na serikali aligoma kuchukua
mshahara wake akitaka nyongeza zaidi kutoka Sh.5 Milioni hadi Sh. 18
Milioni walizokubaliana na mteuzi wake, Rais Kikwete ambapo wakati
akifanya kazi Afrika Kusini alilipwa takribani Sh. 35 milioni.
Hata hivyo, vyanzo vya gazeti hilo kutoka TIC vilidai kwamba Licha ya
Kairuki kugoma kupokea mshahara huo, alijiidhinishia posho kubwa
zilizozidi hata kiwango cha mshahara aliopaswa kupoke kwa ajili ya
safari zisizo na tija za mara kwa mara nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment