Wednesday, March 6, 2013

MWANACHUO WA 'UDSM" ATIWA MBARONI KWA KUMTEKA MTOTO...

Jeshi la Polisi mkoani hapa limewakamata watu wawili wanaodaiwa kumteka mtoto kwa madai ya kupata fidia kutoka kwa wazazi wa mtoto huyo. Taarifa hizo zinasema kuwa mtoto huyo alitoweka nyumbani kwa bibi yake
Februari 27, majira ya saa 4 asubuhi na kwamba baada ya kufanyika kwa operesheni maalumu kutoka kwa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi, alikutwa akiwa mikononi mwa mateka hao.

“Baada ya kupata taarifa, tuliunda timu maalumu na kuwapata watekaji wakiwa wilayani Rombo, mtego wetu ulinasa na kumkamata Nicholaus Lyimo akiwa amejificha katika Kijiji cha Mashimba, Useri Rombo akiwa na mtoto machakani, tulivyompekua tulikuta vyeti vyake vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kisu,” alisema Boaz.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger