Thursday, October 11, 2012

Shitaji mume wala boyfriend kwasababu nahitaji kuwa huru- DIANA EXAVERY


Diana Exavery
Diana Exavery Mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI wa filamu katika tasnia ya filamu swahiliwood Diana Exavery anasema kuwa kazi yake ya filamu anavyoipenda anahitaji kuwa huru zaidi, kufuatia kupata uhuru huo inamradhimu kutokuwa na mahusiano na mwanaume yoyote kwani kwa kukubali kuwa chini ya mwanaume hatakuwa huru na kufanya kazi zake.

.
Diana Exavery
Diana akiwa katika pozi.
Diana Exavery Hashim Kambi
Diana akiwa na Mzee Hashim Kambi katika moja ya filamu.
“Katika maisha yangu nahitaji sana kuwa huru na uhuru najua unapatikana pale mtu anapokuwa hana mahusiano na mwanaume, hilo ndilo naliona kwangu sahihi kwani ninapokuwa huru sipati mtu wa kunisumbua na kunizuia kazi zangu za sanaa kwa ujumla,”anasema Diana.
Msanii huyu alianza kung’ara katika filamu ya Mtunis iliyojulikana kwa jina la Best Wife, baadae alishiriki katika filamu ya Mrembo kikojozi, pia filamu ya Yatima asiyestahili, na hivi karibuni ameigiza katika filamu ya Binti Yangu kama mshiriki kinara, msanii huyo anajinadi kuwa hana mchumba wala mume.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger